Habari na Matukio WhatsApp
Careers & Opportunities

Nafasi za Kazi Wilaya ya Iramba 07-06-2025

Nafasi za Kazi Wilaya ya Iramba 07-06-2025

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Iramba 07-06-2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba anakaribisha maombi ya kazi kwa wananchi wote kwa mwenye sifa ya kuwa mlezi (matron) wa wanafunzi wenye mahitaji maalum Shule ya Msingi Kizega

Kwa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma na marekebisho yake Na. 8 ya mwaka 2014, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba anatangaza nafasi ya kazi kwa waombaji wenye sifa zifuatazo:

Pakua PDF hapa

Sifa za mwombaji

  • Awe Mtanzania
  • Awe jinsia ya kike
  • Awe mwenye moyo wa huruma, upendo na wito wa kukaa na watoto wenye mahitaji maalum
  • Awe tayari kukaa (kuishi) bweni kwa ajili ya kusimamia wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa ukaribu
  • Awe na uzoefu wa angalau mwaka mmoja katika nafasi husika
  • Asiwe amewahi kupatikana na kosa la jinai
  • Awe mwaminifu, mwenye nidhamu na bidii ya kazi
  • Awe na umri kuanzia miaka 25 hadi 45
  • Awe mwenye akili timamu

Kazi na majukumu

  • Kusimamia usafi wa ndani ya bweni, ikiwemo kutandika vitanda, kudeki na kuhakikisha usafi wa wanafunzi wa bweni kwa ujumla
  • Kuwa msimamizi wa karibu wa wanafunzi wenye mahitaji maalum
  • Kuhakikisha kuwa kila aliyeko bwenini ni mwanafunzi halali wa bweni
  • Kuhakikisha kuwa wanafunzi wa bweni wanafuata Sheria za Shule
  • Kupokea wanafunzi kwa utaratibu uliowekwa na kukagua vifaa vyao wanaporipoti shuleni
  • Kushirikiana na mwalimu wa zamu kwenye ugawaji wa chakula cha mchana na jioni kwa wanafunzi wa bweni
  • Kuitisha majina kila asubuhi waondokapo darasani na baada ya vipindi, kwa lengo la kujua idadi ya wanafunzi waliopo bwenini
  • Kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi mwenye kifaa hatarishi ndani ya bweni
  • Kuripoti matatizo ya wanafunzi wa bweni kwa Mwalimu Mkuu
  • Kufanya kazi nyingine yoyote utakayoagizwa na Mkuu wako ambayo haiingiliani na maadili ya kazi
  • Kuhakikisha kuwa wazazi wanaotembelea watoto wao wanakuwa sehemu iliyotengwa na siyo bwenini
  • Utawajibika kwa Mkuu wa Shule

Mambo ya kuzingatia

  • Barua ya maombi iambatishwe na nakala za vyeti vya taaluma kama vinapatikana pamoja na cheti cha kuzaliwa
  • Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Juni 2025
  • Watakaokidhi vigezo vya kuitwa kwenye usaili watajulishwa

Maelezo ya mawasiliano

Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta tu kwa anwani ifuatayo:

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Iramba
S.L.P 155
Kiomboi – IRAMBA

Tangazo hili limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz, ded@irambadc.go.tz
Tovuti: www.irambadc.go.tz

Soma zaidi:

Leave a Comment