Hii hapa orodha ya majina ya walimu walioitwa kazini Jiji la Mbeya 07-06-2025 Waombaji wa nafasi ya kada ya ualimu waliochaguliwa baada ya usaili uliofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26/04/2025 kwa ajili ya kujaza nafasi za ajira ya mkataba kwenye shule za mchepuo wa Kiingereza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya anapenda kuwatangazia waombaji wa nafasi ya kada ya Ualimu kuwa, baada ya kukamilika kwa taratibu zote za usaili, wafuatao wamefaulu na kuchaguliwa kuajiriwa.
Utaratibu wa kuripoti kazini utafanyika kwa awamu mbili kama inavyoonyeshwa kwenye Jedwali Na. 01 na 02 lililoambatishwa.
Aidha, kwa wale waliokuwa wakigombea nafasi za kada tofauti na Ualimu na walioshiriki usaili katika tarehe zilizotajwa, utaratibu wa ajira yao utatolewa baadaye.
Tangazo hili linaambatana na orodha ya majina ya waliochaguliwa kwa kada ya Ualimu.
Waombaji waliochaguliwa wanashauriwa kutembelea mara kwa mara tovuti rasmi ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya kupitia
www.mbeyacc.go.tz
ili kupata taarifa muhimu pindi zinapotolewa.
Kwa waombaji ambao majina yao hayajaonekana kwenye orodha, wanatakiwa kutambua kuwa hawakufaulu usaili huo. Hata hivyo, hawapaswi kukata tamaa – wasisite kuomba tena pindi ajira zitakapotangazwa upya.
Soma zaidi:
Leave a Comment