Habari na Matukio WhatsApp
Utumishi

Walioitwa kwenye Usaili Manispaa ya Moshi 06-06-2025

Walioitwa kwenye Usaili Manispaa ya Moshi 06-06-2025

Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili ajira portal au utumishi 06-06-2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 25/06/2025 hadi 26/06/2025. Aidha, baada ya usaili kukamilika, waombaji kazi watakaofaulu watapangiwa vituo vya kazi.

Pakua PDF hapa

Maelekezo kwa Wasailiwa

Wasailiwa walioteuliwa kuhudhuria usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

Ratiba ya Usaili

Kwanza, fahamu kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili. Vilevile, muda na sehemu ya kufanyia usaili vimeainishwa kwa kila kada.

Mavazi ya Usaili

Pia, kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa mavazi nadhifu.

Utambulisho wa Msailiwa

Kila msailiwa, bila kukosa, anapaswa kuwa na kitambulisho halali kwa ajili ya utambuzi.
Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:

  • Kitambulisho cha Mkazi
  • Kitambulisho cha Mpiga Kura
  • Kitambulisho cha Kazi
  • Kitambulisho cha Uraia
  • Leseni ya Udereva
  • Hati ya kusafiria
  • Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Kijiji/Mtaa

Maelekezo Maalum kwa Kada ya Dereva II

Kwa waombaji wa kada ya Dereva II, ni muhimu kufahamu kuwa wenye leseni ya Daraja E au C wanapaswa kuja na vyeti vya mafunzo ya udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Hata hivyo, wasailiwa ambao hawatawasilisha vyeti hivyo siku ya usaili HAWATARUHUSIWA KUFANYA USAILI.

Uwasilishaji wa Vyeti Halisi

Vilevile, wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia:

  • cheti cha kuzaliwa
  • Kidato cha IV
  • Kidato cha VI
  • Astashahada na kuendelea, kutegemeana na sifa za mwombaji.

Vyeti Visivyokubalika

Aidha, wasailiwa watakaowasilisha:

  • Testimonials
  • Provisional Results
  • Statement of Results
  • hati za matokeo za Kidato cha IV na VI (Form IV and Form VI results slips)
    HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

Gharama za Usaili

Kwa hiyo, kila msailiwa atajigharamia kwa:

  • Chakula
  • Usafiri
  • Malazi

Kuheshimu Ratiba ya Usaili

Pia, kila msailiwa anapaswa kuzingatia tarehe, muda, na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.

Uhakiki wa Vyeti kwa Waliosoma Nje ya Nchi

Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania, wanashauriwa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NACTE au NECTA).

Waombaji Wasioitwa kwenye Usaili

Kwa waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili, watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hata hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

Namba ya Mtihani

Vilevile, wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuhakikisha wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani. Kwa sababu hiyo, namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.

Tahadhari ya Hali ya Hewa

Mwisho wa yote, wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Wilaya ya Ileje ni ya baridi. Kwa hivyo, mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa hiyo.

Soma zaidi:

Leave a Comment