Follow WhatsApp Channel
Careers & Opportunities

Walioitwa Kazini TRA 2025 Ajira 1,896 Zatolewa – Angalia Jina Lako Hapa

Walioitwa Kazini TRA 2025 Ajira 1,896 Zatolewa – Angalia Jina Lako Hapa

Orodha ya majina ya Walioitwa Kazini TRA 2025 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa taarifa rasmi kuhusu mchakato wa ajira wa mwaka 2025. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, jumla ya nafasi 1,896 za kazi zimethibitishwa kujazwa, baada ya kuongeza nafasi nyingine 300 zilizoridhiwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ajira TRA 2025
Angalia Email yako sasa.
Walioitwa Kazini TRA 2025

Kuitwa kazini TRA PDF na tangazo hili hapa

Muhtasari wa Mchakato wa Ajira TRA 2025

Nafasi Zilizotangazwa

  • Nafasi za awali: 1,596
  • Tarehe ya kutangaza: Februari 2025

Maombi ya Kazi

  • Jumla ya waombaji: 135,027
  • Walioitwa kwenye usaili wa kuandika: 113,023

Usaili wa Kuandika

  • Tarehe: 29 – 30 Machi 2025

Usaili wa Mahojiano

  • Waliofuzu kuandika: Walitwa kwenye usaili wa mdomo
  • Tarehe: 12 – 14 Mei 2025
  • Jumla ya washiriki: 6,325

Kuongezwa kwa Nafasi za Ajira

  • Nafasi zilizoongezwa: 300
  • Idadi mpya ya ajira: 1,896
  • Zimekasimiwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26

Matokeo ya Usaili wa Mahojiano TRA 2025

  • Tarehe ya kutangazwa: 28 Mei 2025
  • Njia ya kupata majibu: Kupitia barua pepe zilizotumika wakati wa kuomba kazi

Maelekezo kwa Walioitwa Kazini

Wasailiwa 1,896 waliofaulu wanapaswa:

  • Kufika katika kumbi walizopangiwa
  • Tarehe ya kuripoti: 02 Juni 2025
  • Muda: Saa 1:00 asubuhi
  • Waje na nyaraka muhimu kama ilivyoelekezwa kwenye barua pepe

Taarifa Muhimu kwa Wengine

  • Waombaji 4,429 waliofika kwenye usaili wa mahojiano lakini hawakuitwa kazini:
    • Taarifa zao zitahifadhiwa kwenye kanzidata ya TRA
    • Zitatumika kwa nafasi zitakazojitokeza baadaye

Shukrani Maalum

TRA inamshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia kuongeza nafasi za ajira, hatua ambayo imewezesha kuajiri watumishi zaidi ya ilivyotarajiwa awali.

Mawasiliano ya Zaidi

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia:

  • Tovuti: www.tra.go.tz
  • Namba za simu bila malipo:
    • 0800 780078
    • 0800 750075
    • 0800 110016
  • WhatsApp: 0744 23 33 33
  • Barua pepe: huduma@tra.go.tz / services@tra.go.tz

Soma zaidi:-

1 Comment

Leave a Comment