Nafasi za Kazi Ruangwa – Ajira 14 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa amepokea Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29.04.2025. Watanzania wote wenye sifa zilizo ainishwa hapa chini, wanakaribishwa kuwasilisha maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
Ajira mpya zilizotangazwa
1. Mwandishi mwendesha ofisi II – Nafasi 3
Awe amefaulu Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata Programu za Compyuta za Ofisi kama vile:- Word, Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
2. Dereva daraja la II – Nafasi 11
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (Form Six), Awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Cource) yanayotolewa na Chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.
Jinsi ya kutuma maombi
Barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa na mwombaji wa nafasi za kazi ielekezwe kwa; Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya, 15 Barabara ya Boma, SLP 51, 65682 Ruangwa, Lindi.
Muhimu: Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz na si vinginevyo. Anwani hii inapatikana pia kupitia kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kubofya ‘Recruitment Portal’.
Soma zaidi:-
Leave a Comment