Follow WhatsApp Channel
Careers & Opportunities

Nafasi za Kazi Wilaya ya Madaba 2025

Nafasi za Kazi Wilaya ya Madaba 2025

Nafasi za Kazi Madaba 2025 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba amepokea kibali cha Ajira chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/A/25 cha tarehe 25/04/2025 kutoka kwa katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hizo kama ifuatavyo:-

Ajira mpya zilizotangazwa

1. Mwandishi Mwendesha Ofisi daraja la II – Nafasi 2

Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha, wawe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 80 kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

2. Msaidizi wa Kumbukumbu daraja la II – Nafasi 7

Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada au NTA level 6 katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu, kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, na mwenye ujuzi wa Kompyuta.

3. Dereva Daraja II – Nafasi 5

Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving course) yanayotolewa na chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Jinsi ya kutuma maombi

Barua ziandikwe kwa Anwani ifuatayo;- Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, 38 Barabara ya Kifaguro Magingo, S.L.P 10, 57186 MADABA, SONGEA.

Pakua PDF hapa

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Soma zaidi:-

  1. Nafasi za Kazi Dangote Cement Tanzania
  2. Walioitwa Kazini Walimu, Afya
  3. Nafasi za Kazi BRAC Maendeleo Tanzania
  4. Jinsi ya Kutuma maombi ya Vyuo NACTVET
  5. Nafasi za Kazi KCB Bank Tanzania

Leave a Comment