Nafasi za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imepokea kibali cha ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kibali hiki kina Kumb. Na. FA.97/288/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 pamoja na kibali cha ajira mbadala Kumb. Na. FA.228/613/01G/049 cha tarehe 14/04/2025.
Watanzania wote wenye sifa wanakaribishwa kutuma maombi kwa nafasi zifuatazo:
1. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 11
Majukumu ya Kazi
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kuhakikisha usalama.
- Kuwasafirisha watumishi katika safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo ya gari.
- Kuweka kumbukumbu za safari katika log book.
- Kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kufanya usafi wa gari.
- Kufanya kazi nyingine utakazoelekezwa na msimamizi wako.
Sifa za Muombaji
- Awe na cheti cha kidato cha nne (Form IV).
- Awe na leseni ya daraja C au E.
- Awe na uzoefu wa kuendesha kwa angalau mwaka 1 bila kusababisha ajali.
- Awe amehitimu mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Ngazi ya Mshahara:
TGS B (Mishahara ya Serikali)
2. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4
Majukumu ya Kazi
- Kuorodhesha barua zinazoingia na zinazotoka.
- Kusambaza majalada kwa watendaji na kuyapokea yanaporudi.
- Kuhifadhi majalada kwenye shabaka au kabati maalum.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi.
Sifa za Muombaji
- Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
- Awe na Stashahada (NTA level 6) ya Utunzaji Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Awe na ujuzi wa kutumia Kompyuta.
Ngazi ya Mshahara:
TGS C (Mishahara ya Serikali)
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote ni lazima wawe Raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
- Waambatishe:
- CV yenye maelezo ya kutosha, anwani, namba za simu, na barua pepe inayofanya kazi.
- Majina ya wadhamini watatu wa kuaminika.
- Nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na wakili/mwanasheria.
- Hati za matokeo (slips), Testmonials, Provisional results hazitakubalika.
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU/NECTA/NACTE.
- Wastaafu wa utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali rasmi kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi: 11 Juni 2025.
- Maombi lazima yaambatane na barua ya maombi iliyosainiwa na ipelekwe kwa:
Mkurugenzi
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro
S.L.P 166
MOROGORO
- Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) https://portal.ajira.go.tz
Maombi yasiyowasilishwa kwa mfumo huu hayatazingatiwa.
Leave a Comment