Jinsi ya Kutuma maombi ya ajira kupitia Mfumo wa Maombi ya Ajira wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania (Judiciary Service Commission – JSC Recruitment Portal) kunahitaji kufuata hatua kadhaa rasmi. Hapa chini ni maelezo ya hatua kwa hatua jinsi ya kufanya hivyo:

Hatua za kutuma maombi kupitia Mfumo wa JSC
1. Tembelea Tovuti Rasmi
Nenda kwenye mfumo rasmi wa ajira wa Tume ya Utumishi wa Mahakama:

2. Unda Akaunti (Kama huna)
- Bonyeza kitufe cha “Jisajili” / “Register”
- Jaza taarifa zako binafsi:
- Jina kamili
- Namba ya Kitambulisho (NIDA) au TIN
- Barua pepe inayofanya kazi
- Namba ya simu
- Neno la siri (password)
- Thibitisha usajili kwa kutumia kiungo utachotumiwa kwa barua pepe au namba ya simu.

3. Ingia kwenye Akaunti
- Tumia barua pepe na nenosiri ulilosajili ili kuingia kwenye mfumo.
4. Jaza Wasifu (Profile) Wako
- Jaza taarifa za:
- Elimu yako
- Uzoefu wa kazi
- Vyeti/vielelezo muhimu katika PDF
- Lugha unazozijua
- Referee/wadhamini
- CV na barua ya maombi
- Barua ya utambulisho (kama inahitajika)
- Vyeti vya kuzaliwa, NIDA, n.k.
5. Tafuta Nafasi za Kazi Zilizo Tangazwa
- Nenda kwenye sehemu ya “Nafasi za Kazi” au “Available Vacancies”
- Soma tangazo la kazi vizuri (sifa zinazotakiwa, masharti, deadline)
6. Tuma Maombi
- Bonyeza “Omba” / “Apply” kwenye kazi unayotaka.
- Thibitisha maombi yako kabla ya kutuma.
Maelekezo kwa Waombaji wa Nafasi za Kazi – Tume ya Utumishi wa Mahakama
Sifa za Mwombaji
- Awe Raia wa Tanzania.
- Awe na umri wa miaka 18 hadi 45.
- Awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai wala kufungwa jela.
- Waombaji wenye ulemavu watapewa kipaumbele — tafadhali bainisha aina ya ulemavu kwenye barua ya maombi.
Utaratibu wa Kutuma Maombi
- Maombi yote yatumwe kwa njia ya kielektroniki kupitia tovuti rasmi: www.jsc.go.tz.
(Nakala ngumu hazitapokelewa.) - Barua ya maombi iandikwe kwa: Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 2705, Dodoma.
Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Kujaza Fomu ya Maombi
- Pakia kielektroniki (upload) nyaraka zifuatazo:
- Vyeti vyote vya elimu na mafunzo pamoja na matokeo ya vyeti hivyo.
- Cheti cha kuzaliwa.
- Picha ya rangi (passport size) ya hivi karibuni.
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
- Nyaraka nyingine yoyote kulingana na maelekezo ya fomu ya maombi.
Masharti na Vigezo Muhimu
- Nafasi hizi ni za Ajira Mpya; watumishi wenye ajira za kudumu katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi, vyeti vyao lazima vithibitishwe na TCU/NACTE.
(Maombi bila uthibitisho hayatashughulikiwa.) - Waombaji waliowahi kuachishwa au kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.
- Waombaji wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia masharti haya, maombi yao hayatashughulikiwa.
- Waombaji watakaotoa taarifa za uongo (mfano umri, elimu, historia ya ajira), hata kama wataajiriwa, watatumbuliwa kazini na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
- Waombaji waliopitishwa katika usaili na kuajiriwa:
- Watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania.
- Lazima wawe tayari kupangiwa kituo chochote chenye nafasi wazi.
Mawasiliano kwa Maelezo Zaidi au Msaada
- Simu za maulizo: 0734 219 821, 0738 247 341
- Barua pepe: maulizo.ajira@jsc.go.tz
Mwisho wa Kupokea Maombi
- Tarehe ya mwisho: 17 Juni, 2025.
Soma zaidi:
Leave a Comment