Hii hapa Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania (Angalia hapa) Mkuu wa Jeshi la Polisi anawatangazia vijana waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania kuwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 12/06/2025 hadi tarehe 14/06/2025 kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo.
Vijana waliofanyiwa usaili Dar es Salaam kwenye Vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Polisi wataripoti jijini Dar es Salaam katika uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi (Police Barracks) barabara ya Kilwa nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa Road tarehe 12/06/2025 saa 12.00 asubuhi kwa ajili ya safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
Vijana waliofanyiwa usaili Mikoa ya Tanzania Bara wanatakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliofanyia usaili tarehe 11/06/2025 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupewa utaratibu wa safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
Vilevile, vijana waliofanyia usaili Zanzibar (Unguja na Pemba) wanatakiwa waripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 11/06/2025 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupangiwa utaratibu wa safari.
Aidha, vijana wote waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi wakiwa na vifaa vifuatavyo:
JESHI LA POLISI TANZANIA – MAHITAJI MUHIMU
i) Mavazi na Vifaa vya Michezo na Mazoezi:
- Traki suti (track suit) ya rangi ya bluu yenye ufito mweupe
- Fulana (t-shirt) nyeupe isiyo na maandishi
- Raba (viatu vya michezo)
- Soksi nyeusi
- Bukta mbili (2) za bluu kwa ajili ya michezo na mazoezi
- Sanduku la chuma (tranka) la rangi ya bluu
ii) Vifaa vya Malazi:
- Chandarua cheupe cha duara (sio cha pembe nne)
- Shuka jozi mbili (shuka 4) za rangi ya bluu mpauko (light blue)
- Pasi ya mkaa
- Blanketi moja la kijivu lisilo na maua (sio duveti)
iii) Vifaa vya Kula:
- Kikombe cha plastiki kilichotengenezwa kwa material ya mfupa (cream light)
- Sahani moja aina ya steel dish plate
iv) Vifaa vya Usafi:
- Sururu moja lenye mpini
- Ndoo mbili ndogo
- Fagio la chelewa
v) Bima ya Afya:
- Kadi ya bima ya afya (NHIF) kama anayo
- Au fedha taslimu Tsh. 50,400/= kwa wasio na kadi ya bima ya afya
vi) Nyaraka Muhimu:
- Vyeti halisi vya taaluma (original academic certificates)
- Cheti halisi cha kuzaliwa
- Kadi ya NIDA au namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA)
- Nakala za kadi ya NIDA au namba ya utambulisho wa Taifa za wazazi na watu wa karibu upande wa Baba na Mama (mfano: Baba, Baba mkubwa, Baba mdogo, Shangazi, Mama, Mama mkubwa, Mama mdogo, Mjomba, Babu nk.)
- Passport size 6 (background blue)
- Nakala (copy) 5 kwa kila cheti kilichoainishwa hapo juu
vii) Fedha za Kujikimu
Simu za mkononi haziruhusiwi chuoni, hivyo ni marufuku kuripoti Shule ya Polisi Moshi ukiwa na simu ya mkononi. Yeyote atakayepatikana na simu itachukuliwa kuwa ni utovu wa nidhamu na adhabu yake ni kufukuzwa mafunzo mara moja. Shule itaelekeza utaratibu wa kupata mawasiliano.
Kwa yeyote atakayeripoti Shule ya Polisi Moshi baada ya tarehe 14/06/2025 hatopokelewa na atahesabika amejiondoa mwenyewe kwenye mafunzo.
Orodha ya vijana waliochaguliwa imeambatishwa kwenye tangazo hili.
Soma zaidi:-
Leave a Comment