Follow WhatsApp Channel
Careers & Opportunities

Majina Waliochaguliwa JKT 2025 Kidato cha Sita Selection PDF Shule zote

Majina Waliochaguliwa JKT 2025 Kidato cha Sita Selection PDF Shule zote

Majina Waliochaguliwa JKT 2025 Kidato cha Sita Selection PDF Shule zote Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, anatoa wito kwa vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2025 kutoka shule zote za Tanzania Bara, kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2025.

Tarehe ya Kuripoti Makambini

Vijana wote waliopangiwa wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 28 Mei hadi 08 Juni 2025 katika makambi mbalimbali ya JKT.

Makambi ya JKT Waliyopangiwa Vijana

Vijana wamepangiwa katika makambi yafuatayo:

  • JKT Rwamkoma – Mara
  • JKT Msange – Tabora
  • JKT Ruvu na JKT Kibiti – Pwani
  • JKT Mpwapwa
  • JKT Makutupora – Dodoma
  • JKT Mafinga – Iringa
  • JKT Mlale – Ruvuma
  • JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga
  • JKT Makuyuni na JKT Orjolo – Arusha
  • JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma
  • JKT Itaka – Songwe
  • JKT Luwa na JKT Milundikwa – Rukwa
  • JKT Nachingwea – Lindi

Maelekezo kwa Wahitimu Wenye Ulemavu

Wahitimu wenye ulemavu wa mwili (Physical Disabilities) wanatakiwa kuripoti katika Kambi ya Ruvu JKT, iliyopo Mlandizi, Mkoa wa Pwani, ambayo ina miundombinu maalum ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

Waliochaguliwa kujiunga JKT 2025

Vifaa vya kujitayarisha navyo kabla ya kuripoti

Vijana wanatakiwa kuja na vifaa vifuatavyo:

  1. Bukta ya rangi ya dark blue, yenye mpira kiunoni, mfuko mmoja nyuma, urefu wa magotini, isiyo na zipu.
  2. T-shirt ya rangi ya kijani.
  3. Raba za michezo za kijani au blue.
  4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  7. Track suit ya kijani au blue.
  8. Nyaraka zote muhimu za udahili kujiunga na elimu ya juu, zikiwemo:
    • Cheti cha kuzaliwa
    • Vyeti vya kuhitimu kidato cha nne
    • Nyaraka nyingine muhimu
  9. Nauli ya kwenda na kurudi kutoka makambini.

Jinsi ya kuangalia majina ya waliochaguliwa

Orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa, makambi ya JKT waliyopangiwa, maeneo ya makambi hayo pamoja na vifaa vya kuja navyo, inapatikana katika tovuti rasmi ya JKT

Hatua za Kuangalia Jina na Kambi Ulipopangiwa:

  1. Ingia kwenye tovuti ya JKT.
  2. Ingiza jina au namba ya shule yako ya kidato cha sita.
  3. Utaliona neno “Waliochaguliwa”.
  4. Bofya hapo ili kuona jina lako na kambi uliopangiwa pamoja na Mkoa na Wilaya.
  5. Ili kuona majina yote, pakua PDF ya “JKT 2025” iliyo juu kulia mwa ukurasa huo.

Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, anawakaribisha vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2025 kuungana na wenzao katika Mafunzo ya JKT kwa lengo la:

  • Kujenga Uzalendo
  • Kuimarisha Umoja wa Kitaifa
  • Kukuza Stadi za Kazi na Maisha
  • Kukuza utayari wa kulitumikia na kulijenga Taifa la Tanzania

Soma zaidi:-

2 Comments

  • Mm Nina swali
    Je kama hukubahatika kuchaguliwa jkt Yan kat ya Yale majina yaliyotokewa jina lako likawa halipo , lakini unataka kwenda kwenye hayo mafunzo je utaratibu upoje ?

Leave a Comment