Follow WhatsApp Channel
Admission

Jinsi ya Kutuma maombi ya Vyuo NACTVET (CAS Online Application) 2025-2026

Jinsi ya Kutuma maombi ya Vyuo NACTVET (CAS Online Application)

Jinsi ya Kutuma maombi ya Vyuo NACTVET (CAS Online Application) Jinsi ya kuapply au kufanya maombi ya chuo udahili Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kuutaarifu umma kuwa udahili wa wanafunzi kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2025/2026 umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 28 Mei hadi 11 Julai 2025.

Aina za Maombi ya Udahili

Maombi ya udahili yanagawanyika katika makundi mawili:

Udahili wa vyuo 2025
  • Kozi zisizo za Afya na Sayansi Shirikishi, pamoja na kozi za Afya na Sayansi Shirikishi zinazotolewa Zanzibar:
    Maombi yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.
  • Kozi za Afya na Sayansi Shirikishi – Tanzania Bara:
    Maombi yafanyike kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) unaopatikana kupitia tovuti ya NACTVET

CAS Online application

Mwongozo wa Udahili

Baraza limechapisha Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2025/2026 kinachoorodhesha kozi zote pamoja na vyuo vinavyotoa kozi hizo.

Mwongozo wa udahili wa vyuo vya kati NACTVET

Mwongozo wa udahili wa vyuo vikuu NACTVET

Maelekezo Muhimu kwa Waombaji Wote

  • Mwombaji anapaswa kujihusisha binafsi na mchakato wa maombi.
  • Andika taarifa zako kwa usahihi na umakini.
  • Tunza taarifa utakazopatiwa, hasa msimbo maalum utakaoletwa kupitia SMS.
  • Usitoe taarifa zako binafsi kwa mtu mwingine ili kuepuka usumbufu au udanganyifu.

Mwongozo kwa Wanaoomba Kupitia Mfumo wa CAS (Tanzania Bara)

  1. Unaweza kuomba chuo zaidi ya kimoja.
  2. Ukichaguliwa, utapokea ujumbe wa SMS kutoka NACTVET ukiwa na:
    • Taarifa za chuo ulichochaguliwa.
    • Msimbo (code) wa kuhifadhi na kuwasilisha chuoni.
  3. Baada ya kuwasilisha msimbo huo chuoni, utasajiliwa.
  4. Ukishasajiliwa, tembelea tovuti ya NACTVET kuthibitisha usajili kwa kutumia kipengele cha “Student’s Information Verification”.

Mwongozo kwa Wanaoomba Moja kwa Moja Vyuoni (Kozi zisizo za Afya & Zanzibar)

  1. Unaweza kuomba chuo zaidi ya kimoja.
  2. Ukichaguliwa na chuo, taarifa zako zitatumwa NACTVET kwa ajili ya uhakiki.
  3. Utapokea ujumbe kutoka NACTVET ukieleza kuwa taarifa zako zimehakikiwa pamoja na msimbo (code).
  4. Wasilisha msimbo huo chuoni ili usajiliwe.
  5. Baada ya usajili, tembelea tovuti ya NACTVET na uhakiki taarifa zako kwa kubonyeza “Student’s Information Verification”.

NACTVET inasisitiza kila mwombaji kuzingatia taratibu zilizowekwa ili kuepuka changamoto yoyote katika mchakato wa udahili. Huu ni wakati mzuri wa kuchukua hatua sahihi kwa mustakabali wako wa kitaaluma.

Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti rasmi ya NACTVET katika kiunganishi cha nactvet.go.tz.

Soma zaidi:-

1 Comment

Leave a Comment