Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inaufahamisha umma na wadau wa elimu kuwa Awamu ya Kwanza ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026 imekamilika rasmi. Majina ya waliodahiliwa katika awamu hii yanapatikana kwenye vyuo husika.
Kwa mwaka huu, jumla ya waombaji 146,879 walituma maombi ya kujiunga na vyuo 88 vilivyoidhinishwa na TCU, huku programu za Shahada ya Kwanza zikiwa 894 ikilinganishwa na 856 mwaka uliopita, ikiwa ni ongezeko la programu 38. Aidha, nafasi za udahili zimeongezeka hadi 205,652 kutoka 198,986 mwaka 2024/2025, ongezeko la 6,666 sawa na 3.3%.
Katika Awamu ya Kwanza, jumla ya waombaji 116,596 (sawa na 79.4%) wamepata nafasi ya kujiunga na vyuo walivyoomba. Idadi ya waliodahiliwa inatarajiwa kuongezeka kwenye Awamu ya Pili ya udahili.
Uthibitisho kwa Waliodahiliwa Zaidi ya Chuo Kimoja
Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao kupitia akaunti walizotumia kuomba kuanzia 3 โ 21 Septemba 2025. Uthibitisho huu unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa SMS au barua pepe.
Kwa orodha ya majina ya waliodahiliwa na taarifa zaidi, tembelea tovuti ya TCU: www.tcu.go.tz.
Leave a Comment