Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limetangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa awamu ya pili kwa programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2025/2026.
Kwa mujibu wa NACTVET, jumla ya waombaji 15,526 waliwasilisha maombi kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS). Kati yao, 10,476 wamechaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali, wanawake wakiwa 5,186 (49.5%) na wanaume 5,290 (50.5%).
Waombaji ambao hawakuchaguliwa wanahimizwa kuwasilisha maombi mapya kupitia dirisha la awamu ya tatu litakalofunguliwa 2 – 26 Septemba 2025. Pia, dirisha la uhamisho wa chuo au programu litakuwa wazi katika kipindi hicho.
Kwa matokeo ya udahili na taarifa zaidi, tembelea tovuti ya NACTVET: www.nactvet.go.tz na bonyeza CAS Selection 2025.
Leave a Comment