Portal

Mfumo wa Maombi ya Ajira wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania, Jinsi ya Kutuma maombi

Mfumo wa Maombi ya Ajira wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania, Jinsi ya Kutuma maombi

Jinsi ya Kutuma maombi ya ajira kupitia Mfumo wa Maombi ya Ajira wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania (Judiciary Service Commission – JSC Recruitment Portal) kunahitaji kufuata hatua kadhaa rasmi. Hapa chini ni maelezo ya hatua kwa hatua jinsi ya kufanya hivyo:

JSC Recruitment Portal

Hatua za kutuma maombi kupitia Mfumo wa JSC

1. Tembelea Tovuti Rasmi

Nenda kwenye mfumo rasmi wa ajira wa Tume ya Utumishi wa Mahakama:

Mfumo wa Maombi ya Ajira wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania
Mfumo wa Maombi ya Ajira wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania

2. Unda Akaunti (Kama huna)

  • Bonyeza kitufe cha Jisajili” / “Register
  • Jaza taarifa zako binafsi:
    • Jina kamili
    • Namba ya Kitambulisho (NIDA) au TIN
    • Barua pepe inayofanya kazi
    • Namba ya simu
    • Neno la siri (password)
  • Thibitisha usajili kwa kutumia kiungo utachotumiwa kwa barua pepe au namba ya simu.
Kujisajili Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania
Kujisajili Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania

3. Ingia kwenye Akaunti

  • Tumia barua pepe na nenosiri ulilosajili ili kuingia kwenye mfumo.

4. Jaza Wasifu (Profile) Wako

  • Jaza taarifa za:
    • Elimu yako
    • Uzoefu wa kazi
    • Vyeti/vielelezo muhimu katika PDF
    • Lugha unazozijua
    • Referee/wadhamini
    • CV na barua ya maombi
    • Barua ya utambulisho (kama inahitajika)
    • Vyeti vya kuzaliwa, NIDA, n.k.

5. Tafuta Nafasi za Kazi Zilizo Tangazwa

  • Nenda kwenye sehemu ya “Nafasi za Kazi” au “Available Vacancies”
  • Soma tangazo la kazi vizuri (sifa zinazotakiwa, masharti, deadline)

6. Tuma Maombi

  • Bonyeza “Omba” / “Apply” kwenye kazi unayotaka.
  • Thibitisha maombi yako kabla ya kutuma.

Maelekezo kwa Waombaji wa Nafasi za Kazi – Tume ya Utumishi wa Mahakama

Tuma maombi hapa sasa

Tangazo la nafasi za kazi kwa wote

Tangazo la ajira mpya kwa Technician

Sifa za Mwombaji

  • Awe Raia wa Tanzania.
  • Awe na umri wa miaka 18 hadi 45.
  • Awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai wala kufungwa jela.
  • Waombaji wenye ulemavu watapewa kipaumbele — tafadhali bainisha aina ya ulemavu kwenye barua ya maombi.

Utaratibu wa Kutuma Maombi

  • Maombi yote yatumwe kwa njia ya kielektroniki kupitia tovuti rasmi: www.jsc.go.tz.
    (Nakala ngumu hazitapokelewa.)
  • Barua ya maombi iandikwe kwa: Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama,
    S.L.P 2705, Dodoma.

Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Kujaza Fomu ya Maombi

  • Pakia kielektroniki (upload) nyaraka zifuatazo:
    • Vyeti vyote vya elimu na mafunzo pamoja na matokeo ya vyeti hivyo.
    • Cheti cha kuzaliwa.
    • Picha ya rangi (passport size) ya hivi karibuni.
    • Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
    • Nyaraka nyingine yoyote kulingana na maelekezo ya fomu ya maombi.

Masharti na Vigezo Muhimu

  • Nafasi hizi ni za Ajira Mpya; watumishi wenye ajira za kudumu katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.
  • Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi, vyeti vyao lazima vithibitishwe na TCU/NACTE.
    (Maombi bila uthibitisho hayatashughulikiwa.)
  • Waombaji waliowahi kuachishwa au kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.
  • Waombaji wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia masharti haya, maombi yao hayatashughulikiwa.
  • Waombaji watakaotoa taarifa za uongo (mfano umri, elimu, historia ya ajira), hata kama wataajiriwa, watatumbuliwa kazini na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
  • Waombaji waliopitishwa katika usaili na kuajiriwa:
    • Watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania.
    • Lazima wawe tayari kupangiwa kituo chochote chenye nafasi wazi.

Mawasiliano kwa Maelezo Zaidi au Msaada

  • Simu za maulizo: 0734 219 821, 0738 247 341
  • Barua pepe: maulizo.ajira@jsc.go.tz

Mwisho wa Kupokea Maombi

  • Tarehe ya mwisho: 17 Juni, 2025.

Soma zaidi:

Leave a Comment