Tamisemi

NECTA Selection 2025 Uchaguzi

NECTA Selection 2025 Uchaguzi

NECTA Selection 2025 Yote Unayopaswa Kujua Kuhusu Uchaguzi wa Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 na shule walizopangiwa form five selform mis selform.tamisemi.go.tz.

Katika kila mwaka wa masomo, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu hufanya mchakato wa NECTA Selection kwa ajili ya kuwachagua wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Tano (Form Five) na vyuo vya kati kwa mwaka unaofuata. Mchakato huu hutegemea matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne (CSEE), ambapo wanafunzi waliofanya vizuri hupewa nafasi katika shule mbalimbali za serikali kulingana na ufaulu wao, tahasusi walizochagua, na nafasi zilizopo katika shule hizo.

Jinsi ya kuangalia majina waliochaguliwa kidato cha tano 2025

Uchaguzi wa wanafunzi wa 2025 unatarajiwa kufanyika kati ya Mei hadi Juni, mara baada ya matokeo ya CSEE 2024 kutangazwa. Wanafunzi wanaweza kuangalia majina yao kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI (https://selform.tamisemi.go.tz), ambapo orodha kamili ya wanafunzi waliopangiwa shule huwekwa kwa kila mkoa na halmashauri.

Aidha, mfumo wa selform unatumika kuwasaidia wanafunzi kubadilisha au kuthibitisha tahasusi walizozichagua kabla ya upangaji kufanyika. Ni muhimu kwa wanafunzi kuhakikisha taarifa zao katika mfumo huo ni sahihi.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Kuhusu NECTA Selection 2025

  • Majina ya waliochaguliwa yatapatikana kwenye tovuti ya TAMISEMI https://selform.tamisemi.go.tz
  • Mchakato wa upangaji hufanyika Mei hadi Juni kila mwaka.
  • Wanafunzi hupangiwa shule kulingana na ufaulu na tahasusi walizochagua.
  • Mfumo wa Selform hutumika kubadili au kudhibiti tahasusi kabla ya selection.
  • Wanafunzi wasiopangiwa shule ya serikali wanaweza kujiunga na vyuo au shule binafsi.
  • Ni muhimu kuhakiki taarifa zako za kielimu na tahasusi kupitia mfumo wa selform.
  • Unaweza kutumia simu au kompyuta kuangalia majina yako kwa kuingia kwenye tovuti ya TAMISEMI.

Soma zaidi:-

  1. Tamisemi Selection 2025 – Yote Unayopaswa Kujua
  2. Selection Form Five 2025 to 2026
  3. Selection Form Five 2025 – Jinsi ya Kuangalia Majina
  4. Nafasi za Kazi Bagomoyo Sugar Tanzania

Leave a Comment