Majina ya Walimu Walioitwa Kazini 2025 Call for Wok Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwajulisha waombaji kazi waliopitia usaili kati ya 28 Februari 2024 hadi 12 Januari 2025 kuwa matokeo yao yamechapishwa rasmi. Pia, baadhi ya waliokuwa kwenye kanzidata (database) wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kuibuka.
Jinsi ya Kupata Barua za Kupangiwa Kazi
Waombaji waliopata nafasi wanapaswa kuchukua barua zao katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro – Masjala ya Wazi, ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili. Baada ya muda huo, barua ambazo hazitajulikana zitatumwa kwa njia ya posta.
Masharti ya Kuripoti Kazini
Waombaji waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuripoti kwa waajiri wao ndani ya muda uliotajwa kwenye barua zao za kupangiwa. Muhimu: Leta vyeti halisi (originals) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa uhakiki kabla ya kupatiwa barua rasmi ya ajira.
Kama Jina Lako Halipo?
Usikate tamaa! Ikiwa jina lako halimo kwenye orodha, inamaanisha hukufaulu usaili kwa wakati huu. Tafadhali endelea kufuatilia nafasi mpya za ajira zinazotangazwa mara kwa mara.
Unapochukua Barua Yako, Usisahau Kitambulisho!
Ili kuthibitisha utambulisho wako, njoo na moja kati ya vitambulisho vifuatavyo:
- Kitambulisho cha Uraia
- Hati ya Kusafiria
- Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi
- Kitambulisho cha Mpiga Kura
- Leseni ya Udereva
Kwa maelezo zaidi, tembelea ofisi za Sekretarieti ya Ajira au tovuti yao rasmi.
Tangazo Kamili →
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA ZA WALIMU (01-02-2025)
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA ZA WALIMU (01-02-2025)
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA ZA WALIMU (01-02-2025)
Soma zaidi: Project Engineer at GSM Group Of Companies Tanzania Career